Comments

Hatua ya tume ya uchaguzi kuendesha zoezi la majaribio la uandikishaji wa daftari la kudumu: Limekisikitisha Chadema.


Chama cha demokrasia na maendeleo nchini (Chadema) kimesikitishwa na hatua ya tume ya uchaguzi kuendesha zoezi la majaribio la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa Biometric Voter Registration (BVR) katika baadhi ya maeneo nchini bila kushirikisha vyama vya siasa ambao ndio wahusika wakuu wa daftari hilo huku kikionyesha hofu juu ya ufanisi wa teknolojia hiyo.

Kauli hiyo ya Chadema inatolewa na naibu katibu mkuu John Mnyika katika mkutano wa kwanza wa baraza jipya la wanawake la chama hicho (Bawacha) ambapo kiongozi huyo anasema hatua ya tume ya uchaguzi kushirikisha viongozi wa halmashauri peke yake bila ya kuwepo kwa vyama vya siasa katika zoezi la majaribio la BVR linazua maswali na walakini kutoka kwenye vyama kuhusu mfumo huo na namna ya utendaji kazi wake. 

Mnyika pia akatumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa Bawacha kutoa elimu kwa wanawake kuhusu ushiriki wao katika uchaguzi mkuu ili waweze kuchagua viongozi ambao watakuwa chachu ya maendeleo badala ya kuhadaiwa na rushwa ndogondogo na watu wenye uchu wa madaraka huku makamu mwenyekiti wa Bawacha Hawa Mwaifunga akiwataka wanawake kujiandikisha kwa wingi katika daftari la kudumu ili waweze kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wananyemuhitaji. 

Naye katibu mkuu wa Bawacha Grace Tendega amewataka wanawake nchini kujitokeza kungombea nafasi mbalimbali katika chaguzi zijazo ili kuondoa mfumo kandamizi kwa wanawake hasa katika ngazi za maamuzi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos