Comments

Chris Brown Agongwa Nyundo Nzito , probation yasogezwa mbele


Probation ya Chris Brown kwenye kesi yake ya kumpiga Rihanna imesogezwa mbele zaidi baada ya staa huyo kusafiri bila ruhusa kwenda kufanya show na kushindwa kumaliza masaa aliyopewa kufanya kazi za jamii. 
Mshindi huyo wa tuzo za Grammy, alipanda kizimbani Alhamis hii kwenye mahakama ya Los Angeles nchini Marekani ili kusikiliza ripoti ya maendeleo ya probation hiyo. 

Jaji alimkanya kwa kutumbuiza kwenye show ya hivi karibuni huko San Jose bila kupewa ruhusa ya kusafiri. Wakili wake Mark Geragos alimueleza jaji huyo kuwa ofisi yake ilimshauri vibaya Brown kuwa hakuhitaji ruhusa ya kusafiri.

Brown pia alikuwa anatakiwa kumaliza masaa 1,000 ya kazi za jamii mwishoni mwa January lakini bado amebakiza masaa 200. Ataendelea kuwa huru hadi March 20 ambapo kesi yake itasikilizwa tena na maofisa wa probation kusoma ripoti yao.

Anatarajia kuanza ziara yake na Trey Songz ‘Between the Sheets Tour; Jan. 28 huko Hampton
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos