Mashindano ya Taifa ya mchezo wa Mpira wa meza yanatarajiwa kuanza Fabruari mwaka huu kwa kushirikisha vilabu zaidi ya 10 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi wa Chama cha Mpira wa Meza nchini TTTA, Yahya Mwingilwa amesema michuano hiyo itakuwa ya kutoka ambapo timu zitakuwa zikicheza nyumbani na ugenini.
Mwingilwa amesema, vilabu ambavyo havina vitendea kazi vya mchezo huo, vitatumia shule ya Sekondari ya Kisutu kwa mechi zote yaani za ugenini na nyumbani.
Mwingilwa amesema, katika michuano hiyo wanaamini wataweza kupata vijana wenye vipaji wataingia katika timu ya taifa na kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.






0 comments:
Post a Comment