Comments

Iringa waboresha miundombinu ya kuhifadhia mazao

Wakulima wa mpunga katika kata za Itunundu na Mlenge tarafa ya Pawaga wilayani Iringa wameanza ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi mazao ukiwa ni mkakati wao wa kuanzisha mradi wa kusindika mazao yao ili kuyaongezea thamani
Ujenzi wa mradi huo unajumuisha ghala la kuhifadhia mazao ya mpunga lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,000 ambalo ujenzi wake umekwishakamilika na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 300 pamoja na mashine ya kukoboa mpunga ambapo afisa kilimo wa halmashauri ya Iringa Lucy Nyalu amesema kwasasa wapo katika mchakato wa kujenga jengo la mashine hiyo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Iringa Steven Muhapa amesema pamoja na juhudi hizo kumekuwepo na changamoto nyingi zinazokwamisha maendeleo ya wakulima hao na kusema kuwa viongozi wanaosimamia skimu za umwagiliaji wamejimilikisha skimu hizo kiasi cha kuzuia halmashauri kukagua hesabu za skimu hizo.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ameuagiza uongozi wa skimu za mlenge na magozi kuhakikisha hesabu zao zinakaguliwa na taarifa kupelekwa ofisi ya mkuu wa mkoa kwa lengo la kuhakikisha usalama wa fedha za wanachama wa skimu hizo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos