Rais Barack Obama wa Marekani
Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa, Washington haiko tayari kuingia vitani dhidi ya Russia kwa sababu ya mgogoro wa Ukraine.
Rais Obama ameyasema hayo alipokuwa nchini India na kusisitiza kwamba, vita kati ya Marekani na Russia ni jambo lililo mbali mno. Rais Obama amesema kuwa, Washington itaongeza mashinikizo dhidi ya Moscow na kutumia machaguo yote, isipkuwa chaguo la kijeshi. Marekani na nchi za Ulaya ziliiwekea vikwazo Ruissia tokea mwaka jamna.
Rais wa Marekani ameendelea kuituhumu Russia kwa kuyapatia silaha makundi ya upinzani yaliyoko mashariki mwa Ukraine, tuhuma ambazo zimekanushwa vikali na serikali ya Russia. Matamshi ya Rais Obama yanatolewa katiak hali ambayo, hivi karibuni Sergei Lavrov Waziri wa Mamboya Nchi za Nje wa Russia alisema kuwa, njama za Washington za kutaka Moscow itengwe kimataifa hazitakuwa na tija yoyote ile. Lavrov ameongeza kuwa, matamshi ya Obama yanaonyesha kuwa, Marekani inataka kuudhibiti ulimwengu wote






0 comments:
Post a Comment