Akizungumza hii leo, msemaji wa Mpoto Theatre Gallery Ltd, Dominic Kaura amedai kuwa Mpoto anaweza kuandika vitabu kama waandishi wengine wakubwa wa Afrika.
“Sasa Mpoto yupo tayari kuwa mwandishi wa vitabu vya mashairi kama akina Shaaban Robert, Chinua Achebe na wengine,” amesema Kaura.
“Kwa sasa hivi tumeshaanza mchakato wa kufanya uandishi wa vitabu vya mashairi na baada ya hapo tutaangalia utaratibu ili vitumike kufundishia kwenye mashule mbalimbali. Hivi vitabu vitakuwa vinazungumzia mambo ya kijamii ambayo yatawajenga wanafunzi katika taifa hili na lijalo.”






0 comments:
Post a Comment