P-Square na baba yao wakati wa mazishi ya mama yao
Taarifa iliyowashtua wengi ni kuwa baba mzazi wa mapacha Peter na Paul wa kundi la P-Square la Nigeria, Mr. Moses Okoye aliyefariki dunia November 24 mwaka jana hakuzikwa mpaka sasa.Mzee huyo anatarajiwa kuzikwa leo Ijumaa January 30 huko nyumbani kwao Ifite Dunu, Anambra State.
Haijajulikana bado sababu za kuchelewa kumpumzisha mzazi wao, lakini baada ya Mr. Okoye kufariki mapacha hao waliendelea na maisha yao mengine ya kawaida na kimuziki.
P-Square wamempoteza baba yao ikiwa ni miaka miwili toka waondokewe na mama yao Mrs Josephine Okoye aliyefariki July 11, 2012.






0 comments:
Post a Comment