Comments

TRA: Yalia na ukwepaji kodi na misamaha,

 Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inaweza kukusanya kiasi cha Sh trilioni tano kwa mwaka kutoka kiasi cha Sh trilioni 3.9 za sasa kwa mwaka, endapo misamaha ya kodi na ukwepaji wa kodi utadhibitiwa.

Hayo yamebainishwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade alipokuwa akijibu hoja kwenye kikao na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) 

Alisema ingawa ndani ya miezi sita ya kwanza wameweza kukusanya Sh trilioni 2.17, misamaha ya kodi, ukwepaji wa kodi na uingizaji wa bidhaa kwa magendo, umekuwa ukichangia upotevu wa mapato.

Bade alitaja maeneo mengine yanayopunguza mapato, mbali na misamaha na ukwepaji kodi kuwa ni magendo katika uingizaji wa bidhaa na kuwa TRA inaweza kukusanya bilioni moja kwa mwezi endapo watakamata bidhaa hizo.

“Tumekuwa tukifanya doria, uchunguzi wetu unaonesha kuna meli ambazo zinatia nanga katikati ya bahari na kupakua mzigo,” alisema.

Alisema eneo lingine ni itifaki ambazo nchi imeingia kwenye Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADEC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa zinazoingizwa hazilipiwi kodi.

Aidha, kamati hiyo, imetoa maagizo kadhaa kwa TRA ikiwamo la kuanza utekelezaji wa Sheria Mpya ya VAT iliyosainiwa na Rais.

Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kuendelea kutumika kwa sheria ya zamani kunachangia kuwapo kwa misamaha mingi na kutoa mfano kuwa kwa mwezi Novemba mwaka jana pekee asilimia 41 ya mapato ilitolewa kama misamaha.

Zitto pia alitaka kuharakishwa kwa ripoti ya udhibiti na uingizaji wa sukari, na kuwataka kuja na mapendekezo ya kuhakikisha sukari inayoingizwa nchini inalipiwa kodi, lengo likiwa ni kulinda viwanda vya ndani na kuongeza mapato.

Kamati hiyo pia imeiagiza TRA kuandaa taarifa ya leseni za udereva na matumizi ya mashine za kielektroniki za kutoa risti (EFD) katika tozo mbalimbali na kutaka washirikiane na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutumia mfumo wa ‘flow mita’ ili kuongeza mapato.



Zitto pia aliitaka TRA kutumia timu ya soka ya Taifa Stars katika kutoa elimu ya matumizi ya mashine za EFD.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos