Wenyeviti wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania UKAWA leo wanakutana kwenye mkutano wa faragha kwa ajili ya kujadili ajenda mbalimbali zinazohusu mustakabali wake na hali ya kisiasa nchini humo.
Vinara hao ni Freeman Mbowe wa Chadema, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Emanuel Makaidi wa NLD na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF) wanakutana kwenye mkutano huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kalenda ya UKAWA. Taarifa kutoka ndani ya muungano huo zinadokeza kuwa, mkutano huo utakuwa na ajenda mbalimbali likiwemo suala la kuangalia mgombea wa nafasi ya urais kupitia umoja huo.
Ajenda nyingine alizotaja ni kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa, changamoto ya uandikishaji wa Daftari la Mpigakura, hali ya uchumi na tathmini ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA James Mbatia amesema kama ninavyomnukuu: Ajenda hizo tunazijadili na lengo ni kuhakikisha tunatafuta majibu ya changamoto mbalimbali zilizopo kwa sasa. Aidha Mbatia amesema kuwa, kuhusu suala la mgombea urais wa UKAWA, linaweza kuwa sehemu ya mazungumzo lakini halipo kwenye ajenda.






0 comments:
Post a Comment