Maandamano hayo yaliyofanyika katika chuo cha Faidhiya cha mjini Qum, yamewashirikisha wanafunzi , wahadhiri na wanazuoni kutoka nchi mbalimbali za dunia kulaani kitendo hicho cha kumvunjiwa heshima Mtukufu Mtume (SAW).
Katika maandamano hayo, waandamanaji walitoa nara za kulaani gazeti hilo kwa hatua ya kuthubutu kuchezea hisia za Waislamu zaidi ya bilioni mbili duniani. Hujjatul-Islam Wal-Muslimin, Sayyid Muhammad Saidi, ambaye pia ni msimamizi wa Haram ya Bibi Fatima Maasumah, kwa kusema:
"Maadui wa Uislamu wamefuata mkondo huo baada ya wao kushindwa kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu yaani Uislamu na kwamba hiyo ni juhudi iliyofeli." Jana pia maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran waliandamana mbele ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran kulaani hatua ya gazeti la Charlie Hebdo kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW).






0 comments:
Post a Comment