Barabara ya Morogoro iliyopo kwenye ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka tayari imekamilika na imeshakabidhiwa kwa Tanroad na itaanza kutumika kwa majaribio huku watumiaji wa barabara za mwendo kasi zilizofunguliwa wakitahadharishwa kuwa makini kufuatia ongezeko la ajali katika barabarab hizo ama kutokuzitumia hadi hapo zitakapoanza kutumika rasmi.
Afisa uhusiano wa kampuni ya Strabag inayotendeneza barabara hizo amesema tayari kipande cha kutoka Kimara hadi Posta kimeshakamilika na itaanza kutumika kwa majaribio siku za karibuni huku akibaini uwepo wa matumizi mabaya ya barabara hizo unaosababisha uharibifu mkubwa na kutoa wito kwa watumiaji wa barabarab hiyo kufuata sheria za barabarabani.
Baadhi ya watumiaji wa barabara ya Sinza kupitia Shekilango wameendelea kutoa lawama kwa baadhi ya madereva wanaoshindwa kuwa waadilifu kwa kutoheshimu alama zilizowekwa kufuatia kipande cha Shekilango kufungwa kwa muda wa miezi miwili ili kupisha ujezi wa mzunguko wa magari ya mwendo kasi kitendo kinachosabisha usumbufu mkubwa kwa wajenzi.
Ujenzi wa barabara hiyo uliotekelezwa kwa awamu sita kwenye barabara zenye kilomita 20.9 ambazo ni Kimara-Kivukoni, Magomeni-Morocco na Faya -K/koo ulisainiwa decemba mwakaz 2012 kwa gharama za shilingi bilioni 280.







0 comments:
Post a Comment