Comments

CHAKUA: kimekerwa na kitendo cha bei ya mafuta kushuka lakini bei za nauli bado ziko palepale.

Chama cha kutetea abiria Tanzania Chakua kimeeleza kusikitishwa na kitendo cha bei ya mafuta kushuka lakini bei za nauli bado ziko palepale ambapo kimemuomba waziri wa uchukuzi kuingilia kati suala hilo huku kikitoa siku 90 kwa viongozi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanajenga eneo la kupumzika abiria katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa Chakua Bw Hassan Mchanjama amesema mafuta yanapopanda bei mnufaikaji mkubwa ni wamiliki wa vyombo vya usafiri kwa kupandisha gharama za nauli mara moja halikadhalika yanaposhuka wanaendelea kunufaika huku abiria wakiendelea kuumia.

Kwa upande wake mjumbe mwenyekiti wa bodi ya chama hicho Bw Deo Mfilinge amesema chama hicho kinatoa siku 90 kwa uongozi wa jiji kujenga eneo la kupumzikia abiria katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo vinginevyo kitawaburuza mahakani kwani ni muda mrefu abria wamekuwa wakipata taabu ya kunyeshewa na mvua pamoja na jua kali baada kituo hicho kubomolewa huku wakilipishwa sh. Mia mbili za kuingia ndani ya kituo hicho.

Akitolea ufafanuzi suala hilo kwa njia ya simu afisa habari wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra Bw David Mzirai amesema hatua ya kupunguza gharama za nauli siyo ya kukurupuka kuna mambo mengi ya kuangalia ikiwemo utafiti wa kushuka huko kwa mafuta kunaweza kudumu kwa muda gani.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos