Mkoa wa MOROGORO unatarajiwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yatakayoanza tarehe TATU hadi NANE mwezi ujao katika uwanja wa jamuhuri mjini Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa MOROGORO, Dakta RAJABU RUTENGWE amewaambia waandishi wa habari kuwa maadhimisho hayo yanayotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN yatahusisha maonyesho ya wanawake wajasiriamali pamoja na wadau wengine.
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dk ALLY MOHAMED SHEIN .
Kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka huu ni uwezeshaji mwanamke ,tekeleza wakati ni sasa.







0 comments:
Post a Comment