Comments

Madee, Mh.Temba na Chege wametoa mchango mkubwa katika kumbadilisha Dogo Janja kimaadili


Rapper Dogo Janja amewataja Madee, Mheshimiwa Temba na Chege kuwa ni watu waliombadilisha na kuwa mtu mwema.

Miaka miwili iliyopita Dogo Janja alijiondoa kwenye kundi la Tip Top kwa madai kuwa Madee alikuwa akimdhulumu. Hata hivyo mwaka jana rapper huyo kutoka Arusha aliyeamua kujiunga na Mtanashati Entertainment aliwapigia magoti tena Tip Top kutaja arejee kundini.

Ningependa kila mmoja afahamu kuwa watu hawa, Chege, Madee na Mheshimiwa Temba wamehusika kwa kiasi kikubwa katika kuniweka kwenye njia sahihi katika maisha,” aliandika Dogo Janja kwenye Instagram.

Wamenifanya kuwa mimi nilivyo sasa kwa kunionesha njia sahihi pale watu wema hupita. Hawakutaka kamwe mimi niharibikiwe bali kuwa mtu mzuri kwenye jamii. Hawa ni watu muhimu katika maisha yangu,” aliongeza.

Dogo Janja bado hajatoa kazi mpya tangu arejee Tip Top.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos