Comments

Manyara.: Wakala vipimo na mizani asababisha hasara kwa vyombo vya usafiri

Watumiaji wa nishati ya mafuta ya mitambo mkoani Manyara wamemtaka wakala wa vipimo na mizani kuacha kuendesha zoezi la ukaguzi wa vituo vya mafuta kwa kutegemea matukio na badala yake wamemtaka kuendesha zoezi la mara kwa mara la kustukiza ili kuwabana wamiliki wanaopunguza vipimo vya mafuta kwa lengo la kujinufaisha.

Wakizungumzia utendaji kazi wa wakala huyo aliyeanza kuendesha zoezi la kustukiza la ukaguzi wa lakiri za vituo hivyo hasa katika kipindi hiki cha kushuka kwa nishati ya mafuta wamesema kumekuwepo na mbinu chafu za upunguzaji wa vipimo zinazolenga kuwanufaisha na wao wakipata hasara kwa kuwa hakuna uwiano wa vipimo kulingana na bei, lakini njia pekee itakayowabana ni kuendesha zoezi hilo na sio baada ya kuwepo kwa tukio. 

Nae kaimu meneja wa wakala huyo wa serikali Bw Adamu Saidi amesema kwa sasa wamelazimika kuendesha zoezi hilo la ukaguzi wa lakiri kwenye vituo vya mafuta mara baada ya kupata hofu ya kuwepo kwa uchakachuaji wa vipimo vya mashine za vituo hivyo na kubaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara wachache wenye mashine mpya wakijaribu kupunguza lakini matokeo yake wamekuwa wakiwanufaisha wateja wao.

Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara waliokaguliwa licha ya kupongeza ukaguzi huo,wamesema zoezi hilo limekuwa funzo kwao hasa ikizingatia kuwa baadhi ya mashine zimekuwa zikiwasababishia hasara na kumnufaisha mlaji pasipo kufahamu na hivyo kama lengo ni kumlinda mlaji wakala anapaswa kukgua mara kwa mara.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos