Zoezi la uandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumu la Wapigakura limeanza katika Mkoa wa Njombe, huku likikabiliwa na changamoto nyingi, ikiwamo mashine za Biometric Voter Registration (BVR) kushindwa kutambua watu wenye vidole vyenye michilizi.
kasoro hizo zimekuja siku tatu tangu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kueleza kuwa amenasa nyaraka zinazoonyesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuwa imeshauriwa na mtaalam kutoka Marekani kwamba Tanzania haijawa tayari kwa teknolojia ya BVR.
Uandikishaji huo umeanza jana katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na mamia ya wananchi wamejitokeza katika vituo vya kujiandikisha lakini baadhi yao wamejikuta wakikwama kutokana na mashine za BVR kushindwa kuwatambua kutokana na aina ya vidole walivyokuwa navyo.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema zoezi la uandikishaji limeanza katika mkoa wa Njombe na kwamba viongozi wa tume hiyo wapo kwa ajili ya kusimamia kuhakikisha kunakuwa na mafanikio.







0 comments:
Post a Comment