Asha-Rose MigiroWakati
viongozi wa Kata za Mbalizi katika halmashauri ya Mbeya wamedai kupokea nakala chache za Katiba Iliyopendekezwa, ingawa uongozi wa halmashauri hiyo umesema umegawa nakala saba kwa kila kitongoji.
viongozi wa Kata za Mbalizi katika halmashauri ya Mbeya wamedai kupokea nakala chache za Katiba Iliyopendekezwa, ingawa uongozi wa halmashauri hiyo umesema umegawa nakala saba kwa kila kitongoji.
Ofisa uchaguzi wa halmashauri hiyo, Edward Mwaigombe alisema halmashauri imepokea nakala 17,000 za Katiba Inayopendekezwa.
Alisema nakala hizo zimegawanywa kwenye kata kulingana na ukubwa wa eneo na wingi wa watu.
Mwaigombe alisema halmashauri ya Mbeya ina kata 26 na vitongoji 935.
“Kuna baadhi ya kata zimepata nakala zaidi ya 500 na Kata ya Ilembo itapata nakala 531, kata ya Santiliya 412 na Iwindi nakala 411”, alisema Mwaigombe.
Alisema kuwa ugawaji wa nakala hizo umeangalia uwiano sawa kulingana na ukubwa wa kata na wingi wa watu katika kila eneo.
Awali, viongozi wa Kata ya Utengule Usongwe na Itewe walisema walipata nakala 200 na 156, tofauti na maelekezo ya Serikali ya kupata nakala 300.
Wiki iliyopita, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro alisema kila kata nchini itapata nakala 300 za Katiba Inayopendekezwa ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika kupiga Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni kusambaza nakala hizo kwenye kata 3,800 zilizopo nchi nzima kabla ya kazi ya kupiga Kura ya Maoni kuanza.
“Karibu mikoa yote imepelekewa nakala hizo. Tumeweka utaratibu mzuri ili kila mkoa upate kutokana wingi wa kata zake,” alisema Migiro.







0 comments:
Post a Comment