Comments

Serikali kupitia tume ya taifa ya uchaguzi imeanza kufanya utafiti kuhusu wafungwa nchini kushiriki katika chaguzi mbalimbali hapa nchini.


Serikali kupitia tume ya taifa ya uchaguzi imeanza kufanya utafiti na mazungumzo na taasisi zinazohusika na kundi la wafungwa nchini kushiriki katika chaguzi mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamesemwa bungeni na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama wakati akijibu swali la mbunge wa Nyamagana Mh.Hezekiah Wenje aliyehoji sababu za wafungwa na mahabusu kutoshiriki katika upigaji wa kura.

Ameongeza kuwa wafungwa wenye vifungo vya chini ya miezi sita pamoja na mahabusu watawekewa utaratibu mzuri wa kuwawezesha kushiriki katika upigaji kura kuanzia kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki katika kampeni za uchaguzi.

Ameongeza kuwa hata hivyo kwa mujibu wa ibara ya 5 kifungu cha pili ya katiba hiyo na sheria za uchaguzi,wafungwa wenye vifungo kuanzia miezi sita na kuendelea hawaruhusiwi kupiga kura.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos