Comments

Ufahamu ukweli kuhusu mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi na nini chanzo!

                       
Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi ni tatizo ambalo linaweza kumpata mwanamke yeyote na linapaswa kufahamika mapema ili hatua muafaka zichukuliwe.

  • Laweza kusababisha kifo hatua za matibabu zisipofanyika mapema

  • Mimba zinazotungwa kwenye fallopian husababisha misuli inayozunguka mirija hiyo kushindwa kufanya kazi kutokana na mgandamizo wa mimba inavyokua. Hii husababisha mishipa inayopita karibu na fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo inaweza kuwa chanzo cha kifo kwa mama kama hali isipo dhibitiwa mapema
    .

Kwa kawaida mimba hutunga ndani ya mfuko wa kizazi isipokuwa mara chache huweza kutokea nje ya eneo hili maalumu.

Katika nyumba ya uzazi kuna mirija inayoitwa fallopian ambayo kazi yake ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji; ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi. Hapo ndipo mimba inapaswa kutokea.

Kwa bahati mbaya ama kutokana na hitilafu fulani mimba hiyo inaweza ikatungishiwa kwenye moja ya mirija miwili ya kizazi; upande wa kulia au kushoto.

Ikitokea hivyo, basi itafahamika kuwa mimba hiyo imetungwa nje ya kizazi. Vilevile mimba inaweza ikawa imetungwa nje ya nyumba ya uzazi au mirija. Asilimia 95 ya mimba zinazotungwa nje ya uterasi ama nyumba ya uzazi hutokea kwenye mirija hii ya fallopian. 

Mimba zinazotungwa kwenye fallopian husababisha misuli inayozunguka mirija hiyo kushindwa kufanya kazi kutokana na mgandamizo wa mimba inavyokua. Hii husababisha mishipa inayopita karibu na fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema inasababisha madhara zaidi na hata kifo kwa mama.

Chanzo cha tatizo
Chanzo cha bado hakijajulikana, hata hivyo kuna vihatarishi ambavyo humfanya mwanamke kuwa katika mazingira ya kupata tatizo hili,.

Viashiria hivyo ni pamoja na magonjwa kama maambukizi katika mfumo wa uzazi hasa yale yanayosababisha uvimbe.

Vihatarishi vingine ni kama vile matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba au kuoteana kwa tishu za kwenye nyumba ya uzazi.

Mambo mengine yanayoweza kusababisha mimba kutungwa nje ya nyumba ya uzazi ni uvutaji wa sigara. Nikotini iliyoko ndani ya tumbaku huchochea kusinyaa kwa mirija ya ya fallopian na hata kusababisha mirija hiyo kuziba.

Jambo jingine ni upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani unaohusu mirija ya fallopian na kusababisha mrija husika kusinyaa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos