Comments

‘vita imeanza’: Ni wazi kuwa Ivan Ssemwanga, aliyekuwa mume wa Zar anataka kulipiza kisasi kwa Diamond kwa kumchukua Wema,


Ivan Ssemwanga, aliyekuwa mume wa Zari The Bosslady na aliyezaa naye watoto watatu ameanza kurusha mashambulizi kwa adui yake namba moja, Diamond Platnumz.
                                Kuanzia Kulia: King Lawrence, Ivan Ssemwinga na Wema Sepetu
Mfanyabiashara huyo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini huenda akalipiza kisasi kwa Diamond anayetarajia kupata mtoto wake wa kwanza kutoka kwa Zari kwa mbinu ya ‘jino kwa jino’ ama zile za ‘kama noma basi iwe noma’. 
Awali Lawrence alipost picha nyingine hiyo chini akiwa kwenye eneo lile lile ambalo Wema alipiga picha
.Picha iko hivi, Wema Sepetu kumbe yupo nchini Afrika Kusini ambako hata hivyo hatufahamu ameenda kufanya nini. Mshkaji wa karibu wa Ivan, King Lawrence (Yule mchizi aliyempa ofa Diamond ya $40,000 ili aachane na Zari), ameshare picha kwenye mtandao wa Instagram akila bata na Wema huku Ivan akiwpo pia.

Kwenye picha hizo, Lawrence anaonekana akiwa amekaa juu ya mapaja ya msichana asiyejulikana na pembeni yake yupo Ivan huku Wema aliyevaa kigauni kifupi cheusi akiwa kulia kwake. 

Lawrence pia amepost video kadhaa akiwa kwenye club hiyo na kuziandika ujumbe wa mfumbo ambao unaeleweka wazi kuwa unawaendea Zari na Diamond. “Rich Gangstas – What goes around comes around,” ameandika. “Oh Z*** get out of the way,” ameandika kwenye video nyingine ambayo unasikika wimbo wa Ludacris, Move Bitc*.

Ni mapema sana kuhitimisha kuwa Ivan anataka kulipiza kisasi kwa Diamond kwa kumchukua Wema, lakini ni wazi kuwa kambi yake inataka kupeleka ujumbe ulio wazi kwa Chibu kuwa ‘vita imeanza’.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos