Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana, Black Stars wamezawadiwa magari mapya aina ya ‘2015 Jeep Grand Cherokee’
Magari hayo 30 yametolewa na kampuni ya Tanink Ghana ambayo ni wasambazaji wakuu wa Jeep nchini humo kama zawadi kwa kufanikiwa kuingia fainali kwenye kombe la AFCON 2015 ambapo Ivory Coast ilichukua ushindi.
CEO wa kampuni hiyo, Roger Klogo alidai kuwa serikali haijahusika kununua magari hayo.
Gari moja inauzwa kwa $76,000 ambapo magari 30 yamegharimu $2,280,000.
Pamoja na Grand Cherokee, kila mchezaji alipewa kitita cha $25,000 na shirika la taifa la mafuta la nchi hiyo, (GNPC).







0 comments:
Post a Comment