Ripoti kutoka Algeria zinasema kuwa, tatizo la wasichana wengi kukosa waume lizaidi kuongeza nchini humo na inakadiriwa kuwa, wasichana milioni 11 kati ya jamii ya watu milioni 40 wa nchi hiyo hawana waume na wamekuwa wakiishi maisha ya ukapera.
Wataalamu wa masuala ya kijamii na kisiasa wanaonya kuwa, mwenendo huo ni hatari kwa usalama wa jamii hasa kutokana na kutokuweko mpango jumla wa kuwashajiisha vijana wa nchi hiyo kuoa.
Takwimu zinaonesha kuwa, suala la mabinti kutoolewa na kuishi maisha ya ukapera limegeuka na kuwa tatizo la kijamii nchini Algeria ambapo mabinti zaidi ya milioni 11 wenye umri wa zaidi ya miaka 25 hawajaolewa. Kwa mujibu wa takwimu hizo, milioni 5 kati yao wana umri wa miaka 35 jambo linaloonesha kuongezeka umri wa ndoa nchini Algeria. Hali ya ugumu wa maisha inatajwa kuwa sababu ya vijana kukwepa kuoa na hivyo kupelekea kuongezeka idadi ya wasichana ambao hawajaolewa.







0 comments:
Post a Comment