Comments

Waziri wa ujenzi Dr John Magufuli amewataka wasafirishaji kwa njia ya barabara kuzingatia sheria zinazotawala uendeshaji kuilinda miundombinu


Serekali imewataka wasafirishaji kwa njia ya barabara kuzingatia sheria zinazotawala uendeshaji wa shughuli hiyo,ili kuitunza na kuilinda miundombinu inayo jengwa kwa garama kubwa.

Waziri wa ujenzi Dr John Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kukagua ujenzi wa kilomita themanini na tisa za barabaraya lami ya Manyoni-Itigi- Chaya mkoani Singida inayojengwa na kampuni ya china ya Synohydro kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni miamoja na kumi ikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya nchi.

Katika hatua nyingine Dk Magufuli amewata wamiliki wa magari makubwa kuhakikisha wanaacha kubeba uzito mkumbwa na badala yake wabebe tani hamsini na sita zilizo pangwa na serekali ilikunusuru uharibifu wa barabara.

Awali mtendaji mkuu wa wakala wa barabara Mhandisi Parick Mfugale amesema pamoja na barabara hiyo kuchelewa zaidi ya mwaka mmoja kulingana na mkataba, lakini ujenzi kwasasa umekamilika kwa asilimia tisini na tano jambo ambalo lina tia moyo.

Dk.Magufuli amefanya ziara ya siku moja mkoa ni Singida kukagua maendeleo na changamoto za miradi ya ujenzi wa barabara, ikiwa ni mojawapo ya barabara za lami zinazo jengwa nchini kote na serekali ya tanzania zenye urefu wa kilomita kumina moja elfu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos