Mchezaji nyota wa Real Madrid ya Uhispania na Ureno Christiano Ronaldo ndiye binadamu maarufu zaidi duniani kwenye Facebook.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 amempiku Mwanamuziki maarufu Shakira mwenye wafuasi zaidi ya milioni 107. Ronaldo anawafuasi 107,096,356 wakilinganishwa na 107,087,100 Shakira
Ronaldo aliweka rekodi kwa kuwa mchezaji maarufu zaidi duniani alipotimiza wafuasi milioni 100 mwezi Oktoba mwaka uliopita. Nyota huyo wa Real Madrid alijiunga na mtandao wa kijamii wa Facebook mwaka wa 2009.







0 comments:
Post a Comment