Comments

Je, wajua kuwa kula karanga na viazi unaweza kulewa kama umekunywa pombe? soma hapa ujue

Watu wengi wangependa kulewa bila kutumia hela zao kununua
vileo. Lakini Nick Hess kutoka ulaya anahitaji tu kiwango kidongo cha viazi kulewa chakari.

Nick anakabiliwa na hali nadra ya afya maarufu kama "Auto- Brewery Syndrome".

Hii inamaanisha kuwa yeye anaweza kulewa chopi kwa kula kifuko kizima cha viazi karanga.

Mkewe ameiambia BBC kuwa wakati mwengine huwa wanaweza kuwa chumbani wakila na kustarehe tu kwa kutizama Televisheni kisha mumewe anaanza kuwa mwenye matusi makali na kuropokwa maneno yenye aibu hata mbele ya wageni wao.

Awali walikuwa anamkaripia kwa utovu wa adabu lakini baada ya kipindi kirefu cha kuvumilia aligundua kuwa hakuwa ameondoka wala kunywa tembo kisri.

Alimpeleka hospitalini na ni huko alikoambiwa kuwa maskini mumewe alikuwa ''ni mgonjwa'' wala sio mlevi kama alivyodhaniwa.Chachu

"Auto- Brewery Syndrome"

Hii ni hali ambayo huwezesha tumbo la mgonjwa kugeuza chakula chenye wanga (Cabohydrate) tumboni kuwa na uwezo wa kulewesha kwani tumbo lake hutoa chachu (Yeast) kwa wingi ambayo hufanya chakula tumboni kugeuzwa tembo kwa haraka mno.

Katika hali yake Bwana Hess, tumbo lake linatoa Chachu maradufu mara 3 zaidi ya mwili wa kawaida.

Mkewe anaeleza jinsi alivyokuwa akisaka chupa za tembo zilizofichwa ndani ya nyumba bila mafanikio.

Kwa muda mrefu hakufahamu hasa kilichomkumba akisema kwamba anajipata mgonjwa bila sababu kwa kuumwa na tumbo na kichwa.

Marafiki na familia walianza kumtuhumu kwamba alikuwa mlevi kiasi .

Aliiambia BBC: "halikuwa jambo la kawaida, mara nyingi ningetamani kula viazi lakini punde tu nilipokula tu najiskia mlevi na kuamka asubuhi nakuwa na mchafuko wa roho.Nick Hess kutoka ulaya anahitaji tu kiwango kidongo cha viazi kulewa chakari

Watu walifikiria kwa ni mlevi licha ya kutotumia kileo chochote, ni wakati tu mkewe alipomnasa kwa kanda ya video na kudhibitisha kwamba hatumii vileo.

Mkewe, Daren Daw, anasema Hata baada ya kupimwa hospitalini kwa muda mrefu, shida hiyo iligunduliwa baada ya kumpa mmewe chakula kizito chenye wanga.

Mwaka wa 2010 alipewa glasi moja ya tembo lakini alipopimwa damu iligundulika kuwa tumbo la bwana huyo lilikuwa limechubua kileo sawana mtu aliyegonga glasi 7 za pombe kali ya Vodka.

Kwa sasa anapewa dawa ya kupambana na vimelea na kutumia vyakula kiasi venye wanga lakini bado anajipata melvi mara moja au mbili kwa mwezi
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos