Comments

Mkuu wa mkoa wa mbeya Abasi kandolo ameupongeza mfuko wa maendeleo ya jamii GEPF kwa kuboresha huduma kwa wateja wao

Mkuu wa mkoa wa mbeya abasi kandolo
Mkuu wa mkoa wa mbeya Abasi Kandolo ametoa wito kwa mfuko wa maendeleo ya jamii kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili wajiunge na mfuko huo kutokana na huduma zao kuwa bora tofauti na mifuko mingine ya jamii. 
Ameyasema hayo katika semina iliyoandaliwa na mfuko wa jamii (GEPF) katika ukumbi wa hill view hii leo hapa mjini kuwataka viongozi wa mifuko ya maendeleo ya jamii kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na kwa wateja wao kiujumla.

Kandolo ameupongeza mfuko huo wa jamii kwa kuboresha huduma zao kwa wateja kwa kuwapa huduma stahiki tofauti na miaka ya nyuma kwa mikakati waliyo jiwekea ya kuwajali wanachama na kuwataka ( GEPF) kuwa makini kwa kufuatilia mafao ya wanachama ,kujenga mahusiano mazuri na wanachama pamoja na wadau wengine kama vile makundi ya wafanya biashara,bodaboda ,wafanya biashara wadogo wadogo,wakulima na wafungaji.

Vile vile Kandolo amewasihi wanachama wa mfuko huo wanaokopa fedha au wanao chukua kiasi cha mafao yao kuyatumia kwa ajili ya shughuri za kimaendeleo.
                                         picha ya pamoja na waandishi wa habari baada ya semina
Aidha meneja wa mfuko wa maendeleo ya jamii( GEPF) Tanzania Aloyce B.Ntukamazina amesema kuwa,matarajio ya mda mfupi ya mfuko huo ni kuweka fao la afya,fao la uzazi ,urafiki wa posta,na mpango hiari kwa watu wanaoishi nje ya nchi (diaspora).

Hata hivyo meneja wa mfuko huo nyanda za juu kusini Ramadhani Sosora amesema kuwa,changamoto zinazo wakabili kama mfuko ni uelewa mdogo kwa wananchi kuhusu umhimu wa kujiwekea akiba,ukosefu wa kipato cha uhakika,mipango ya upatu,na utamaduni wa kujiwekea akiba bado upo chini kwa wananchi wengi.

Kwa upande wao maafisa utumishi waliohudhuria semina hiyo kutoka wilaya mbalimbali mkoani mbeya wamesema kuwa,wanaushukuru mfuko huo kwa semina hiyo na wataenda kuwafikishia taarifa watumishi wengine ambao hawajahudhuria semina hiyo faida ya kuweka akiba ya uzeeni
                                                  afisa masoko GEPF
Picha na moris mwaweza 
Habari barick tuja
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos