Comments

Kiongozi wa Muslim Brotherhood kunyongwa

Mahakama moja nchini Misri imethibitisha hukumu ya kifo ya kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie na watu wengine 13 kwa
kupanga mashambulizi dhidi ya serikali.

Pia mahakama hiyo imemfunga maisha raia mmoja mwenye uraia wa Marekani na Misri na watu wengine 36.

Badie alipewa hukumu hiyo mnamo mwezi Machi na pia anakabiliwa na mashtaka mengine.

Hatahivyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Mamia ya watu wamehukumiwa kifo katika msako dhidi ya wanachama wa kundi hilo kufuatia kuondolewa kwa rais Mohammed Morsi mwaka 2013.

Hatahivyo ,kufikia sasa ni mtu mmoja pekee aliyenyongwa.

Uamuzi huo wa mahakama ulitangazwa moja kwa moja na runinga za taifa hilo.

Hukumu hizo ni za mwisho katika kesi ambayo viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood walishtakiwa kwa kuwachochea wanachama wa kundi hilo kuanzisha ghasia dhidi ya serikali kufuatia maandamano ya mwaka 2013.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos