H.Baba amethibitisha kuwa mke wake Flora Mvungi ni mjamzito na hivyo wanatarajia kupata mtoto wa pili.
Akizungumza leo hii, H. Baba amesema miongoni mwa mafanikio aliyopata mwaka jana ni pamoja na kumpa ujauzito mwingine mke wake.
“Faida ya mwaka jana ni mwana mama Flora Mvungi kujaa tena,” alisema. “Nikwambie kitu kimoja mimba huwa haipigiwi kelele, wala mimba sio kwenye magazeti. Mimi mimba huwa inaonekana, nawafundisha vijana wenzangu mimba sio kelele kwenye magazeti wala kwenye media hapana na mimba inaonekana baba. Flora Mvungi ameonekana kwahiyo ana mimba tayari. Kwahiyo nawafundisha vijana wenzangu ukicheza mechi vizuri utapata matokeo mazuri.”






0 comments:
Post a Comment