Rapper Mabeste amedai kuwa amemaliza tofauti zake na label yake ya zamani, B’Hits Music Group.
Akiongea na mtangazaji wa kituo cha redio cha Kitulo FM cha Makete, Njombe, Ergo Elly, rapper huyo alisema aliufuata uongozi wa B’Hits na kuwataka kumaliza tofauti zao.
“Mwaka jana nilikuwa nimegombana na menejimenti yangu ya hapo mwanzo B’Hits so nikaona mwaka huu nianze na hii nyimbo ‘Usiwe Bubu’ ya amani na watu wengi walikuwa wanajua tumegombana na ni kweli tulikuwa tumegombana lakini all in all ugomvi umeshaisha,” alisema.
“Ni kwa sababu niliwafuata nikamaliza hii bifu na kisa cha kuwafuata ni kwa sababu ndani ya maisha kuna mtu wa karibu alitaka kuiua familia yangu , mke na mtoto na ndani yake nikaweza kusamehe sasa nikaona why not kama nimeweza kumsamehe huyu mtu ambaye alitaka kuua my family ni mtu wangu wa karibu sana nimemsamehe kwanini nishindwe kuwasamehe hawa marafiki ambao tumekuwa nao miaka mingi!
Mabeste aliongeza: Haya ni mambo ya familia ambayo sikupenda kuyazungumzia sana kwa sababu yalishapita, nilishasaheme, nikiyazungumzia tena nitakuwa naweka mambo nje. Mimi nilienda B’Hits nikamtafuta Pancho tumalize hii issue kwa sababu mimi nipo na menejimenti yangu mwenyewe na yeye yupo kwenye menejimenti yake kwahiyo hizi bifu kati yetu tuzitoe kwa sababu hazina maana, kila mtu anafanya ma






0 comments:
Post a Comment