Comments

Mbeya City Wainyima Raha Simba




SIMBA fungu la kukosa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya timu hiyo jana kukosa mkwaju wa penalti na kufanya kupata kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mbeya City katika mechi ya ligi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


Ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, Simba ilikuwa na uwezo wa kusawazisha bao la pili baada ya mwamuzi Abdallah Kambuzi wa Shinyanga kuizawadia mkwaju wa penalti baada ya Yusuph Abdallah wa Mbeya City kumuangusha Jonas Mkude eneo la hatari, lakini mchezaji Nassoro Masoud ‘Chollo’ alikosa kwani shuti alilopiga liligonga mwamba.


Katika mechi hiyo, Simba ndio ilianza kupata bao la kuongoza lililofungwa na chipukizi Ibrahim Ajibu aliyepiga shuti kali la adhabu ndogo akiwa umbali wa mita 27 na mpira huo kumshinda kipa wa Mbeya City, David Buruani na kutinga wavuni na matokeo kubaki hivyo hadi mapumziko.


Kipindi cha pili, Mbeya City walioonekana kucharuka na kasi ya mashambulizi yao iliwasaidia kupata bao la kusawazisha lililofungwa kwa shuti kali la mbali na Ahmed Kibopile, na bao hilo lilionekana kuwapa nguvu vijana wa kocha Juma Mwambusi na dakika ya 90 Yusufu Abdallah aliifungia timu yake bao la ushindi kwa penalti baada ya kipa Manyika Peter kumwangusha Raphael Alfa ndani ya eneo 18.
Uamuzi huo ulionekana kulalamikiwa na wachezaji wa Simba wakidai kuonewa lakini mwamuzi hakuyumba na kuamuru penalti ipigwe. Simba ambayo katika mchezo huo ilimkosa nyota wake Emmanuel Okwi aliyezimia kwenye mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Azam FC, ilionekana kupotea katika kipindi cha pili hasa baada ya kocha Goran Kuponovic kufanya mabadiliko ya kuwatoa Danny Sserunkuma na Simon Sserunkuma ambao nafasi zao zilichukuliwa na Elias Maguli na Ibrahim Twaha.
Katika kipindi hicho cha pili ambacho kilitawaliwa zaidi na Mbeya City, Simba walilazimika kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa kutumia mabeki wa pembeni, Chollo na Mohamed Hussein ambao nao kwa jana hawakuwa kwenye kiwango chao cha kawaida.
Katika dakika ya 77, mshambuliaji Paul Nonga alikosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa Manyika Peter lakini shuti lake lilitoka nje nakuwa golikiki.
Wakati mchezo huo ukiwa katika dakika za ziada, mwamuzi Abdallah Kambuzi aliizawadia Simba penalti baada ya kiungo wake Mkude kuangusha ndani ya eneo la hatari na Abdallah, lakini mpigaji Chollo alipoteza mkwaju huo baada ya shuti lake kugonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani na sekunde chache mwamuzi akamaliza mchezo na kumuacha Chollo akimwaga machozi uwanjani.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos