Rapper Joh Makini kutoka Weusi Kampuni, amesema kuwa kwa Tanzania ina waongozaji wawili tu wa video ambao anaweza kuwapa dhamana ya kazi zake.
Joh amesema ingawa kuna wengine wadogo ambao wanachipukia lakini Nisher na Adam Juma ndio waongozaji wa video anaowakubali Tanzania.
“Mimi kwa sasa hivi naona kama kuna ma-director wawili ambao mimi ninaweza nikawapa dhamana ambao ni Nisher na Adam Juma, wapo up-coming directors kama Hanscanna wanakuja sijui kama ulishawai kuona video zao? Lakini mimi nimeshaziona, niwazuri vijana wadogo lakini wanajituma kweli kweli wale kama wakipata support, nafikiri wanakwamishwa na equipment,” alisema Joh Makini.






0 comments:
Post a Comment