Comments

Picha: Dj D-Ommy wa Times FM afanya tour Kenya

DJ wa kituo cha Times FM, D-Ommy yupo nchini Kenya alikoenda kujitangaza zaidi. 


DJ D-Ommy (katikati) akiwa na crew ya Citizen TV akiwemo Willy M Tuva (mwisho kulia) na Fundi Frank (wa pili kulia)

Ommy amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha kuwa mwaka huu ‘anavuka boda’ zaidi.


DJ D-Ommy akihojiwa na Tuva

Jumatatu hii alikuwa kwenye studio za Citizen TV akihojiwa na mtangazaji Willy M Tuva kwenye kipindi cha Mseto. Kipindi kinaruka Jumanne.


Ommy akionesha ujuzi wake wa kucheza na turn table

“Wenzetu hawalali, wanafanya kazi sana na Djs wa huku wanaheshimiwa sana,” Ommy ameiambia Bongo5 kuhusu alichojifunza huko.

“Pia nashukuru mixxtape zangu zinafanya poa huku, hasa ‘Washa Washa’, ndo watu wanaijua sana,” ameongeza.

Ommy amesema Madj wengi wa Tanzania hawajulikani Kenya kwakuwa hawajitangazi. “Wengi wanawajua watangazaji tu wa huko kama wakina Salama but kwa Djs ilikua ni mimi tu sababu ya Mixxtape za Online.”

“Uwezo wangu wengi wamekubali ninachokifanya. Jumanne hii nina Show Club Tribeka kwenye Usiku wa Wakilisha East Africa. Na pia nitakua na Interview ya Radio ya Citizen pia.”

Katika hatua nyingine DJ D-Ommy amewataka mashabiki wake kujiandaa kwa mixtape yake mpya ya ‘Valentine’s volume 2′
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos