DAR ES SALAAMU
waziri wa ujenzi na miundo mbinu DK.JOHN MAGUFULI ameendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuwataka watu wanaofanya biashara kando ya barabara jijini dar es salaam waondoke na watakao kaidi kutekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua za kishera .
waziri huyo ametoa agizo hilo katika ziara ya ukaguzi wa barabara zinazojengwa jijini dar es salaam na kusisitiza kuwa hata kama serikali itajenga barabara nyingi na zikigeuzwa kuwa sehemu ya kuwa sehemu ya kufanyia biashara tatizo la msongamano wa magari halitakwisha.
magufuri amesema inashagaza kuwa mabilioni ya fedha yanatolewa kwa ajili ya matumizi barabara lakini baadhi watu wanazihujumu.
hata hivyo mkuu wa mkoa wa dar es salaamu MHE. SAIDI MECK SADIKI ameziagiza halmashauri zote za mkoa wa dar es salaam kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara na kama hazitafanya hivyo hatozipitisha bajeti zao.






0 comments:
Post a Comment