DODOMA
Mkutano wa kumi na nane wa bunge la jamuhuri ya mungano wa tanzania umeanza leo mjini dodoma, mkutano huo utajadiri ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikal,i taarifa za kamati za kudumu za bunge na miswada mitatu inayotarajiwa kusomwa na kupitiwa na mkutano huo.
mkutano huo utaanza kwa kumuapisha mwanasheria mkuu wa serikali mh george mcheche masaju na miswaada inayotaajiwa kuwasilishwa ni ule wa sheria ya usimamizi wa kodi wa mwaka 2014,mswada wa sheria ya takwimu ya mwaka 2013 na mswada wa marekebisho ya sheria mbalilbali namba mbili wa mwaka 2014 .
pia bunge litajadili taarifa za udhibiti na ukaguzi wa hesabu za serikali zilizowasilishwa katika mkutano wa kumi na tano wa bunge kuhusu hesabu zilizokaguilwa za serikali kuu,serikali za mitaa na mashirika ya umma kwa mwaka 2012 na 2013 ambapo serikali itatolea majibu baadhi ya hoja.
aidha kamati teule ya bunge iliyoundwa kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi ,kilimo, mifugo, maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi,mifugo, maji na uwekezaji itapewa nafasi ya kuwasilisha taarifa yake ambapo taarifa hiyo itajadiliwa bungeni.






0 comments:
Post a Comment