Comments

Tanzania: Rais Kikwete awateua mawaziri wapya 8 na manaibu watano

Rais Jakaya kikwete wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.

Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano, 
tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.

Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.

Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene

Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos