Comments

Wanablogu Hatarini Saudi Arabia

Mwanablogu Raif Badawi ana majeraha ambayo hayawezi kumruhusu kupewa adhabu nyingine

Saudi Arabia imeahirisha adhabu ya kumchapa viboko mwanablogu Raif Badawi kwa sababu ya afya yake.

Mwanablogu huyo ambaye pia ni mwanaharakati aliyeanzisha mtandao wa 'Forum Liberal Saudi Network' ambao sasa umefungwa na serikali, alitarajiwa kuchapwa viboko 50 hadharani baada ya sala ya Ijumaa hii leo.

Mwezi Mei mwaka jana, alihukumiwa miaka 10 jela na kuandikiwa adhabu ya mijeledi 1,000 kwa kuitusi dini ya kiisilamu pamoja na kutoitii sheria.

Bwana Badawi alipokea awamu ya kwanza ya viboko Ijumaa iliyopita huku kesi yake ikisababisha tuhuma kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali ya Saudia.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos