Comments

Profesa Mark Mwandosya:Kutatua Tatizo La Umeme Tanzania


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Sudan jana amtembelea moja ya miradi mikubwa ya kuzalisha umeme kwa kutumia mabwawa ambao unaendeshwa na Kampuni ya Merowe Dam Electricity Company.

Mradi huu ambao uko Kaskazini mwa Nchi ya Sudan umejengwa kwa gharama ya USD 2.0 milioni ambapo Serikali ya Sudan imechangia 30% na zilizobaki ilikuwa misaada na mikopo kutoka kwa wafadhili
Mradi umejengwa kando kando ya Mto Nile na una uwezo wa kuzalisha 1,250 megawati unachangia 60% hadi 70% ya mahitaji ya nishati ya umeme nchini Sudan. Mkurugenzi Mkuu wa Merowe Dam Electricity Company, Bw. Mahgoub Eisa Khalil amemtembeza Waziri na Ujumbe wake sehemu mbalimbali za mradi kama inavyoonekana katika picha zifuatazo:



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ( wa sita toka kushoto) na ujumbe wake wakiwa na Uongozi wa Bwawa la Umeme la Merowe wakiwa mbele ya Kitoleo cha Maji(Spillway) Wengine kutoka kushoto ni: Ngusa Izengo,Katibu wa Waziri;David Mziray kutoka Sumatra;Grace Nsanya;kutoka Wizara ya Maji;Wallace Chiwawa,TCAA;Hassan Amin Mohammed Ahmed Omer,Mkurugenzi wa Usalama wa Bwawa;Ashraf Mustafa,Meneja wa Uendeshaji;Mahgoub Eisa Khalil,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Umeme,Merowe;Felix Ngamlagosi,Mkurugenzi Mkuu,EWURA;Mhandisi Mustafa Hussein,Afisa Mwandamizi,Wizara ya Maji na Umeme,Sudan;Meneja wa Kituo; na Clemence Kichao kutoka TCRA.


Prof.Mwandosya alipata nafasi ya kuongea na Waandishi wa Habari wa Sudan walioongozana na ujumbe wake huko Merowe,Sudan,akiwa mbele ya moja ya Piramidi za Merowe.Piramidi za Merowe zilijengwa zaidi ya miaka 7000 Kabla ya Ukristo,na ni zamani zaidi kuliko zile za Misri.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos