Comments

Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu amesema walioua wanajeshi watakiona


Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu amesema wote waliohusika na mashambulizi dhidi ya msafara wa majeshi ya Israel watalipa gharama ya waliyoyafanya.

Israel imesema wanajeshi wake wawili waliuawa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na Hezbollah katika mpaka kati Lebanon na Israel.

Mara tu baada ya shambulio lililosababisha wanajeshi hao wawili kuuawa,Israel ilijibu mapigo kwa kufyatua makombora kwenda Lebanon.

Nayo majeshi ya Kulinda amani ya Umoja wa mataifa nchini Lebanon limesema mwanajeshi wao mmoja aliuawa.

Akitoa onyo dhidi ya walihusika na shambulizi hilo Netanyau amesema wote waliohusika lazima wawajibike.

"Yoyote aliyehusikia na shambulizi atalipa gharama. Kwa nyakati fulani Iran kupitia Hezbollah imekuwa ikijaribu kuanzisha mashambulizi ya kigaidi dhidi yetu kutoka katika milima ya Golan. Tutajibu kwa nguvu zetu zote majaribio ya mashambulizi haya. Serikali ya Lebanon na utawala wa Rais wa Syria Rais Bashar una utahusika na matokeo yoyote kutokana na mashambulizi yanayoanzisa kutoka kwenye mipaka ya nchi yake dhidi ya taifa la Israel. Kwa matukio yote haya mpango wetu ni kulilinda taifa la Israel. Tunachozingatia ni usalama wa taifa la Israel na watu wake. Ndio maana tutachukua hatua na tataendelea kuchukua hatua."Amesema Netanyahu.

Nayo Hezbollaha kwa upande wake imekiri kufanya shambulio hilo kwenye msafara wa majeshi ya Israel kwenye mpaka kati ya Lebanona Israel. Hezbollah imesema shambulio hilo ni majibu ya mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel siku kumi zilizopita ambayo yaliua Jenerali wa Iran na wapiganaji sita wa Hezbollah katika mji wa Queneitra nchini Syria. Msemaji wa Hamas huko Gaza Sami Abu Zuhria mesema shumbulio hilo dhidi ya Israel lilikuwa la haki.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos