Comments

Wizara Ya Afya Zanzibar, Imewataka Madaktari Kuendeleza Taaluma zao

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Muhammed Shein, ameutaka uongozi wa Wizara ya Afya visiwani humo kutowazuia wafanyakazi wake kujiendeleza kielimu.

Dk Shein, aliyasema hayo wakati akifungua jengo jipya la upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo katika hospitali ya Mnazi Mmoja visiwani hapa, ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema anashangazwa na baadhi ya watendaji wa wizara hiyo kuwazuia wafanyakazi kujiendeleza kitaaluma, wakihofia kuwa nafasi walizonazo zitachukuliwa na watakaorejea kutoka masomoni.

Alisema, anapenda kuona wafanyakazi wa wizara hiyo na wizara nyingine kutoridhika na elimu walizonazo, badala yake kujiendeleza ili kuifanya nchi kuwa na watalamu waliobobea katika fani tofauti.

“Endapo mfanyakazi anataka kwenda kusoma iwe Tanzania au nje ya Tanzania, mpeni ruhusa akasome na kama wizara haina fedha basi iandikieni barua kwa Serikali Kuu kuomba fedha hizo” alisema Dk Shein.

Pia, aliiagiza wizara hiyo kuhakikisha kuwa huduma nzuri za uchunguzi katika hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja inapatikana ili wananchi waweze kupata matibabu bora.

Alisema katika kuhakikisha hospitali hiyo kuzidi kupata maendeleo ni lazima kubadilika na kuwa makini katika utendaji wa kazi zao bila ya kumuhofia mtu yoyote.

“Kama kupewa maneno au kubezwa katika kuleta maendeleo ni kufa, ningekuwa mimi nishakufa zamani kwani hadi leo wapo wanaoniona mimi mkorofi, lakini sitaki upumbavu nataka kuona mabadiliko katika mambo ya maendeleo” alisisitiza Dk Shein.

Alisema ili kuhakikisha mabadiliko ya maendeleo yanapatikana ni lazima hospitali hiyo kuwa na uongozi madhubuti.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Mohammed Saleh Jidawi, alisema huduma za upasuaji katika kituo hicho zimeanza mwaka 2004 na wameshapokea wagonjwa 2,625 wenye matatizo ya uti wa mgongo na ubongo na kati ya hao wagojwa 580 wamewashafanyia upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos