Comments

MBEYA:Wakala wa majengo Tanzania walazimika kutumia nguvu kurejesha nyumba ya serikali na kuwaondoa wapangaji

                      
Wakala wa majengo Tanzania,TBA,wamelazimika kutumia nguvu kuwaondoa wapangaji kwenye nyumba ya serikali ambayo mfanyakazi mstaafu wa wizara ya ujenzi aliyetajwa kwa jina la injinia Mwikola anayeishi jijini Dar es salaam kwa sasa anadaiwa alijimilikisha na kuipangisha kwa manufaa yake binafsi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 bila kufuata utaratibu.

Wakizungumza wakati wa zoezi la kuziondoa familia nne ambazo zilikuwa zimepanga kwenye nyumba hiyo, maofisa wa wakala wa nyumba Tanzania TBA wamesema kuwa nyumba hiyo ni mali halali ya serikali ambayo imekuwa ikitumika kinyume cha utaratibu na kwamba kabla ya kuchukua uamuzi wa kuirejesha kwa nguvu serikalini, wamefuata taratibu zote za kisheria.

Mmoja wa watumiaji wa nyumba hiyo Semeni Magoma, ambaye amedai kuwa ni shemeji yake na mmiliki wa nyumba aliyemtaja kwa jina moja la injinia Mwikola, amekiri kuwa ameishi kwenye nyumba hiyo kwa muda mrefu na kwamba hata baada ya kupata notisi kutakiwa kuondoka kwenye nyumba hiyo aliwasiliana na shemeji yake ambaye alimuhakikishia kuwa nyumba hiyo aliinunua na ni mali yake halali, hali ambayo iliwafanya wapuuze wito wa kutakiwa kuhama kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos