Comments

Ruvu shooting Yaichapa 2-1 STAND UTD

RUVU Shooting imeendelea kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, baada ya kuifunga Stand United mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.


Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Juma Nade dakika ya tano, kabla ya Hamisi Thabit kuisawazishia Stand dakika ya 53.

Yahya Tumbo ndiye aliyeihakikishia pointi tatu za nyumbani Ruvu hivi leo, baada ya kufunga bao la pili na la ushindi dakika ya 89.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Yanga SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos