Wafanyabiashara mkoani iringa wamelalamikia uamuazi wa serikali kupandisha kodi kwa asilimia mia moja wakieleza kuwa ongezeko hilo halifanani na hali halisi ya kibiashara na litaathili mahusiano kati ya wafanyabiashara na mamlaka ya mapato nchini TRA.
Malalamiko hayo yametolewa na wafanyabiashara hao mbele ya mkuu wa mkoa wa iringa Bibi.Amina Masenza kwenye kikao kilichoandaliwa na mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kutafuta suluhu ya kero mbalimbali za wafanyabiashara mkoani hapa ambapo wameshauri serikali kushirikisha wadau katika maamuzi hayo ili kuondoa migongano kati ya wafanyabiashara na mamlaka ya mapato nchini.
Kwa upande wake meneja wa TRA mkoa wa iringa Bibi.Rozaria Mwenda amesema pamoja na kukusanya kodi jukumu la mamlaka hiyo pia ni kutoa elimu kwa wadau na kuwataka wafanyabiashara hao kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo ili kuondoa usumbufu.







0 comments:
Post a Comment