Comments

DAR ES SALAAM: Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) linatarajia kutangaza bei mpya za umeme

                                           Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) linatarajia kutangaza bei mpya za umeme ambazo zitakuwa na unafuu kwa wananchi baada ya kushuka kwa bei ya mafuta nchini, wakati wowote kuanzia leo.
 
Kutangazwa kwa bei hiyo ni agizo la Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene la kuwataka (TANESCO) kuangalia uwezekano wa kushusha gharama za umeme baada ya kushuka kwa bei ya mafuta ili kuwagusa moja kwa moja wananchi wa kawaida.

Aidha Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) nayo imetakiwa kuangalia namna itakavyoweza kushusha bei za nauli baada kushuka kwa gharama za mafuta.

Simbachawene ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, baada ya mkutano wa pamoja kati ya wadau na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wizara hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos