Comments

Jeshi la polisi wilayani Mvomero mkoani Morogoro limezuia maandamano ya wakulima wa miwa Turiani waliotaka kuandamana

Jeshi la polisi wilayani Mvomero mkoani Morogoro limezuia maandamano ya wakulima wa miwa Turiani waliotaka kuandamana kwa lengo la kulalamikia kiwanda cha Mtibwa kushindwa kulipa madeni yao kwa muda mrefu.
Wakizungumza kwa jazba wakulima hao wamesema kuwa hawaoni sababu ya jeshi la polisi wakiwa na silaha kuwazuia kufanya maandamano ya kudai haki yao kwani ni muda mrefu wanalalamikia kiwanda hicho bila majibu.

Kwa upande wa diwani wa kata ya Mtibwa Lukas Mwakambaya baada ya kuhojiwa na jeshi la polisi kwa saa kadhaa katika kituo cha polisi Mtibwa amesema jeshi la polsi limezuia maandamnao hayo kutokana na kukosa kibali ambapo amesema haokuona sababu ya jeshi la polisi kutumia silaha na kuweka utepe kuzua wakulima wasiingie kiwandani kudai haki yao kwani walifanya biashara na kiwanda na wana haki ya kulipwa jasho lao.
Nae meneja wa kiwanda cha Mtibwa Sugar Ahmed Yahaya amekiri madai ya wakulima hao kuwa ni ya msingi na ameshindwa kulipa kwa wakati kutokana na kuharibika kwa soko la sukari la ndani baada ya kupata hasara kufuatia uingizaji holele wa sukarti bila ushuru ambapo ameahidi tarehe 20 mwezi huu atafanya malipo yote ya wakulima.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos