Comments

Boko Haram wajikusanya katika ngome ili kuandaa mashambulizi.

Ripoti kutoka Nigeria zinasema wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Boko haram wanakusanyika kwenye ngome yao ya Gwoza na
kuimarisha nguvu zao kutoka maeneo mengine.

Chanzo kimoja cha kijasusi ambacho kinaangalia hali ilivyo kimeiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba vikosi vya jeshi vinakaribia kwenye mji na wanamgambo huwenda wanajiandaa kuulinda mji wa Gwoza, ambao ni moja ya miji mikubwa ya mwisho wanayoidhibiti huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Chanzo hicho kinasema vikosi vya kundi la Boko haram vinasafiri kuelekea Gwoza kutoka kwenye makambi yao ya kisiasa yaliyo karibu na msitu wa sambisa. Gwoza inapatikana kiasi cha kilomita 135 kusini ya mji mkuu wa Borno, Maiduguri.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos