Wanachama wakuu wa bunge la wawakilishi nchini Marekani wamemwandikia barua Rais Obama wakimhimiza kutoa silaha hatari kwa Ukraine ili kuisaidia kupambana na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
Barua hiyo imevitaja vitendo vya Urusi kuwa dhihaka inayokiuka sheria ya kimataifa.Wanajeshi wa Ukraine wakikabiliana na waasi huko mashariki mwa Ukraine
Wamemtaka Obama kuidhinisha kusafirishwa kwa silaha za kujilinda haraka iwezekanavyo.
Obama alikuwa amesema kuwa Marekani inachunguza uwezekano wa kutoa silaha kwa Kiev iwapo juhudi za kidiplomasia hazitafaulu.







0 comments:
Post a Comment