Hukumu ya kifo kwa watuhumiwa wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi iliyotolewa na mahakama kuu imeibua hamasa na mitazamo
tofauti wananchi ambao pamoja na kupongeza hatua hiyo wamesema wanachosubiri sasa ni kuona ngazi zinazohusika zikitekeleza hukumu hiyo.
tofauti wananchi ambao pamoja na kupongeza hatua hiyo wamesema wanachosubiri sasa ni kuona ngazi zinazohusika zikitekeleza hukumu hiyo.
Wananchi hao wamesema ili adhabu hiyo iweze kuwa na tija na kuwa fundisho kwa wengine ni vyema utelezaji wa hukumu iliyotolewa ufanyike haraka na jamii ione huku wengine wakitaka kesi zinazohusiana na mauaji ya albino zitenganishwe na kesi zingine ili zisichukue muda mrefu.
Katika hatua Bi.Ester Mahawe ambaye ni mkurugenzi wa shule ya Intel School ya mkoani arusha amejitolea kuwasomesha watoto wawili wenye ulemavu wa ngozi ambao mdogo wao aliuawa hivi karibuni huko geita.
Akitangaza azima yake hiyo Bi.Ester amesema baada ya kutafakari kwa muda amebaini kuwa anachoweza kusaidia ni kuwalea na kuwasomesha watoto hao,Shija Bahati (11) na Aseri Bahati (2) kuanzia elimu ya awali hadi darasa saba.







0 comments:
Post a Comment