Comments

Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara .

Serikali Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara, ambapo watu wa familia ya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani.

Mjane wa marehemu Miriam,akizungumza kupitia njia ya simu kutoka Paris amesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji yake.

Bwana Sankara aliuawa mnamo mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaore kuchukua mamlaka.

Blaise Campaore aling'atuliwa mamlakani katika mapinduzi ya raia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita.

Serikali mpya inayoongozwa na Michael Kafando ,imesema kuwa italiangizia swala hilo wakati ilipochukua hatamu.

Mwili wa Sankara ulizikwa katika kaburi lisilotambulika katika makaburi yaliopo mashiriki mwa mji wa Ouagadougou.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos