Comments

Jux na Vanesa Mdee waweka hadharani uhusiano wao wa kimapenzi

Jux amethibitisha uhusiano wake na muimbaji huyo wa ‘Hawajui’ kwenye mahojiano na kituo cha redio baada ya
kipindi kirefu wawili hao kuwa wamekuwa wakikanusha kuwa na uhusiano.

Nshaconfess siku nyingi tu. Mwanzo nilikuwa nakataa kwasababu ilikuwa bado unajua first time unakutana na mtu na lazima itafika time mtasema now it’s a time naweza nikasema tu tuko hivyo. Mimi sipendi unasema leo hivi halafu kesho yanatokea mambo mengine, lazima uone kwamba sasa naweza nikasema,” alisema Jux.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo alizungumzia pia kuhusu nyumba yake.

Muimbaji huyo amekuwa akipost picha ya nyumba yake hiyo yenye ghorofa moja na kuwaacha watu wengi na maswali kibao ni wapi amepata uwezo wa kujenga nyumba hiyo ilhali si msanii aliye busy na show kama wengine na hana biashara kubwa anayoifanya kumwezesha kuwa na utajiri huo. Hata hivyo kupitia mahojiano na mtangazaji wa Kings FM, King Davidy, Jux amesema nyumba ni ndoto aliyokuwa nayo hata kabla hajajulikana kwenye muziki na hadi nyumba hiyo imefika hapo imetokana na desturi aliyokuwa nayo ya kutunza fedha kwa miaka mingi.

Watu hawawezi kujua mimi nimeanza muda gani hadi kufika pale, unaweza kukuta hata miaka 10 iliyopita. Kwa hiyo sio kitu cha jana na ni kitu cha taratibu, unapata laki tano unaweka, unapata milioni mbili.. sababu nyumba haiozi kama chakula, ni kitu ambacho kinaenda taratibu. Sio kama mimi tajiri sana na nina hela, hizo ni dreams tu,” alisema muimbaji huyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos