Comments

Leo ni siku ya wanyama na mazao ya porini duniani, pinga mauaji holela ya wanyama hao kama tembo

Leo ni siku ya wanyama na mazao ya porini duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka umakini zaidi katika kushughulikia vitendo vya uhalifu dhidi ya maliasili hiyo.

Katika ujumbe wake, Ban amesema biashara haramu ya wanyamapori na bidhaa zitokanazo na viumbe hivyo ikiwemo ndovu, magogo na kifaru, imekuwa ikiibuka na mbinu mpya kila uchao na hata kuzidi ile ya usafirishaji haramu wa binadamu na dawa za kulevya.

Amesema kushamiri huko kunapigiwa chepuo na rushwa na uongozi dhaifu akiongeza kuwa kuna ushahidi thabiti wa kuhusika kwa mitandao ya kihalifu iliyopangwa na vikundi vilivyojihami.

Ban amesema biashara hiyo haramu siyo tu inakwamisha utawala wa sheria bali pia unatishia usalama wa taifa na ni kikwazo kikubwa kwa juhudi za wanavijiji na jamii za watu wa asili za matumizi endelevu za maliasili.

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu ametaka umakini wa kushughulikia uhalifu huo akitaka ushiriki wa jamii zote zinazohusika na matumizi ya maliasili hizo kwa ajili ya dawa, chakula, ujenzi, samani, urembo na nguo.

Amesema endapo usimamizi wa sheria utakwenda sambamba na ushirikishi wa jamii nzima kutawezesha kumaliza tatizo la matumizi haramu ya bidhaa za porini.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

New Hope Company. Powered by Blogger.

Facebook

Wazo Hai

Search This Blog

Blog Archive

Flickr

Social Share

Featured
Featured

Labels

Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

TANGAZA NASI HAPA

East Africa Radio Live Here

Tags

Fashion

Sponsor

Videos